Bawazir Aeleza Uhusiano Wake Na Ali B Na Beef Na Wasanii Wa HipHop
Baada ya maswali kuzagaa mtaani kuhusu uhusiano wake na babake Ali B, msanii Bawazir amefunguka mengi kuhusu swala hilo pamoja na mengi ikiwemo beef na wasanii wa hip hop, kuhusu yeye kuacha shule na story yake ya kimaisha tangu azaliwe. Kulingana na Bawazir ni kwamba uhusiano wake na Ali B uko sawa kwa sasa ila kila mmoja anafuata shughuli zake, nikimnukuu … “Ki ukweli mimi siko na Ali B, sikuwahi kumuona tangu nilipozaliwa. Nilimjua nikiwa na miaka kumi na nne, nikajaribu kumthamini lakini sikupata ile support. Kuna wengi wana pesa na hawajaona babazao, mimi nashkuru nilikuja nikaonyeshwa kwa hivyo hanisaidii lakini hiyo ilinipa changamoto saa hii naweza kujisimamia” Bawazir amesema. Kuhusu masomo, Bawazir amesema kwamba kwa sasa anasubiri kukalia mtihani wa kidato cha nne baada ya kujilipia ada ya tuition kisirisiri. Bawazir amezungumzia kila kitu kwa kina katika mahojiano yake na Kelvin.
0 Response to "Bawazir Aeleza Uhusiano Wake Na Ali B Na Beef Na Wasanii Wa HipHop"
Post a Comment