Susumila Hawajibikii Mtoto Vilivyo Ndio Maana Nimemshtaki-Kibibi Afunguka
Baada ya kuachana na msanii Susumila, Muigizaji Kibibi Salim ameweka wazi sababu maalum iliyosababisha hadi wawili hao wakaachana. Kulingana na Kibibi, ni kwamba matatizo katika ndoa yao yalianza kitambo saana yakakithiri hadi kufikia kiwango cha kutoweza kuvumilana tena. ”Tulikosa kuvumiliana mimi na yeye ndio maana hii kitu haiku work,ila angenivumilia na mimi nikamvumilia basi tungeishi pamoja hadi miaka hamsini hadi sitini”. Kibibi amesema huku akieleza ya kwamba Susumila hawajibiki vilivyo kama baba ndio maana akampeleka kortini huku akidai ya kwamba lazima Susumila awajibikie watoto wake inavyotakikana. Msikilize akizungumzia sababu za kutalakiana na Susumila, sababu za kumshtaki, uhusiano wake na Ruth (mpenzi wa zamani wa Susumila), na akieleza kama ni kweli wameungana na Ruth kumshtaki Susumila…Na Je Susumila arekebishe nini ndio warudiane?
0 Response to "Susumila Hawajibikii Mtoto Vilivyo Ndio Maana Nimemshtaki-Kibibi Afunguka"
Post a Comment