-->
Mswazi Masauti Aanika Kilichomtoa SwaRnB

Mswazi Masauti Aanika Kilichomtoa SwaRnB

Alipochukuliwa na SwaRnB ilikua ni wazi ya kwamba Masauti alikua ametoboa kimziki kwani anayemiliki recording label hio ni producer mkongwe ambaye ana uzoefu mkubwa katika sanaa kwani hata yeye ndiye aliyewatambulisha Necessary Noize, Kalamashaka, GidiGidi, MajiMaji nawasanii wengi tajika. Mashabiki walitarajia hit baada ya hit lakini kwa kipindi cha mwaka mmoja project iliyoweza kuzaliwa kutoka kwa ndoa hio ya kikazini moja tu! Mashabiki walianza kulalamika kusema ya kwamba msanii huyo anapotezwa kwani kipaji alichonacho na ukizingatia ya kwamba yuko na management hafai kua msanii wakufanya project moja kwa mwaka. Mapema mwezi huu ndio tulipata fununu ya kwamba Masauti hayupo tena SwaRnB, akatugusia tu kwa kutudokezea ya kwamba kuna vitu havikua vinaenda kama ilivyotarajiwa ndio maana wakasitisha mkataba. Hatimaye Masauti ameamua kufunguka kwa kina kilichopelekea mkataba huo kufika kikomo, vilevile ameeleza mipango yake na Kigoto na management flani inayomnyemelea katika mahojiano yake na Kelvin Jilani/ Mswazi Masauti Aanika Kilichomtoa SwaRnB.


0 Response to "Mswazi Masauti Aanika Kilichomtoa SwaRnB"

Post a Comment

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel